Usiku wa sifa, wa raha na nuru,
Alipozaliwa Mwana m-takatifu na mwema,
Mwana ndiye Mungu, Mwana ndiye Mungu.

Usiku wa sifa, wachunga bondeni,
Nuru iliwaogofya, malaika wakaimba,
Kazaliwa Mwana, Kazaliwa Mwana.

Usiku wa sifa, neema na amani,
Upendo na ukombozi umewafikia wote
Kwa Masihi Yesu, kwa Masihi Yesu.